Makonda ampa shavu Ismail Aden Rage

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda ameunda Uongozi wa muda (Interim Committee) baada ya kuusimamisha Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kuusimamisha Uongozi wa sasa wa kamati hiyo kufuatia malalamiko ya baadhi ya Wagombea waliokuwa wakiwania nafasi mbalimbali za uongozi wa TOC kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi uliotangazwa kufanyika April 12, 2026.

Katika Uteuzi huo, Makonda amemteua Ismail Aden Rage kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo huku Dkt. Steven Mabagala akiwa ndiye Makamu Mwenyekiti.

Wengine ni Amina Mfaume (Katibu) na Wajumbe ni Kesi Said Mohammed, Jemedari Said, Asma Hilal na Queen Siraki.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons