Yanga waamua kuhamia Zanzibar

Na Prince Hoza

Uongozi wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, umeiandikia barua ZFA kutaka kuutumia uwanja wa Amaan, Zanzibar kama uwanja wake wa nyumbani baada ya serikali kuzipiga stop Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kaimu katibu mkuu wa Yanga, Baraka Deusdetit ameiambia Mambo Uwanjani kuwa Yanga wameamua kuiomba ZFA kuutumia uwanja wa Amaan kama uwanja wa nyumbani.

Yanga na Simba zilitakiwa na Bodi ya Ligi kuchagua uwanja wa kuutumia katika mechi zake za Ligi kuu bara, endapo Yanga itakubaliwa kuutumia uwanja wa Amaan, timu zote itakazokutana na Yanga katika Ligi kuu bara zitalazimika kupanda boti kwenda visiwani Zanzibar

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons