Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SIKIA MANENO YA VICENT BOSSOU KUHUSIANA NA WASHAMBULIAJI WA LIGI KUU TANZANIA BARA .

Na Mwandishi Wetu

BEKI wa kati wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Vincent Bossou raia wa Togo ameibuka na kusema hakuna mshambuliaji anayemuumiza kichwa kwa sasa kwenye Ligi kuu bara, Bossou alicheza vizuri na kuwauzia washambuliaji wa kati wa Simba katika mchezo uliomalizika Jumamosi iliyopita uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mlinzi huyo ameiambia Mambo Uwanjani kuwa hajaona washambuliaji wenye uwezo wa kumpita, katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya kufungana bao 1-1, Simba ilipata bao lake kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja, hivyo washambuliaji wake watatu Ibrahim Ajibu, Laudit Mavugo na Fredric Blagnon walishindwa kupenya mbele ya beki huyo anayefahamika kama Kaka jambazi

" Kwa sasa hapa Bongo sijaona mshambuliaji ambaye anaweza kunitisha wala kunifanya nimuwaze kukutana naye kwasababu wote nawaona wa kawaida na wengi wao wanaongea na tunapokutana nao wanakuwa na Viwango vya kawaida tofauti na wanavyoongea.


Angalia hata katika mchezo uliopita yule Mavugo wa Simba alitamba kwamba tungepata ushindani Kutoka kwake na kila mtu aliona jinsi ambavyo tulifanikiwa kazi yetu.", alisema mlinzi huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Togo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa