COUTNHO AJIPELEKA SIMBA
Kiungo wa Yanga raia wa Brazil Andrey Coutinho huenda akavaa uzi mwekundu na nyeupe msimu ujao kufuatia taarifa zake za kutaka kutemwa ndani ya Yanga hivyo na yeye ameanza maandalizi ya kujiunga na Simba msimu ujao.
Coutinho ambaye anasifika kwa mipira wa faulo na kona, yuko mbioni kujiunga na Simba kwa dau la kawaida ili kuwaumiza Yanga ambao wametangaza kumtema, rafiki wa karibu wa mchezaji huyo amedai mipango ya swahiba wake kujiunga na Simba ni mikubwa na muda wowote anaweza kumalizana nao.
Pia watu wa Simba wameonyesha kumuhitaji kiungo huyo kutokana na umahiri wake aliounyesha katika ligi hiyo, Coutinho anakumbukwa kwa magoli yake mazuri ya faulo likiwemo lile aliloifunga Azam FC wakati timu yake ya Yanga ikilala 2-1.
Mbrazil huyo aliyejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu uliomalizika akiwa na sambamba na Wabrazil wenzake makocha Marcio Maximo, Leonardo Neiva na mshambuliaji Geilson Santana Santos 'Jaja'. mambo uwanjani inafahamu kila kitu kuwa Coutinho ni miongoni mwa wachezaji waliotangazwa kutemwa na Yanga na yuko mbioni kutua Simba.
Pia timu nyingine zinazomuwania Mbrazil huyo ni pamoja na Stand United ya Shinyanga na Mbeya City ya Mbeya