BUHARI: ASEMA USHINDI WAKE NI WA KIDEMOKRASIA

Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Nigeria Muhammadu Buhari anasema kuwa ushindi wake unamaanisha kuwa taifa hilo linafuata mfumo wa kidemokrasi.

Buhari alimshinda mpinzani wake Goodluck Jonathan,kwa kura millioni 2 idadi ambayo wachanganuzi wanasema kuwa itazuia harakati zozote za kuanzisha kesi.


Ni mara ya kwanza kwa rais wa taifa hilo kushindwa katika uchaguzi.

Bwana Buhari ,kiongozi wa zamani wa kijeshi alichukua mamlaka mnamo mwaka 1980 kupitia mapinduzi.

Hatahivyo alifanya kampeni za kidemokrasia kwa lengo la kutaka kusafisha siasa katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Katika hatua ya kidemokrasia,rais anayeondoka Goodluck Jonathan alimpigia simu Buhari kukubali ushindi na vilevile kutoa taarifa akiwataka wafuasi wake kukubali matokeo.

Mabadiliko mengine makubwa yaliyosababisha kuvurugika kwa kiasi kikubwa kwa ratiba ya VPL yalianza kufanywa mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar Januari 13.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA