SIKIA HII:- KIBIBI YAHYA AMPOKONYA WIMBO WA "NO DISCUSSION" SALHA WA HAMMER Q!!.

Na Kais Mussa Kais

Kibibi Yahya ni muimbaji wa kutegemewa wa bendi ya Maja's Modern Taarab iliyo na maskani yake manzese jijini Dar!, katika siku za nyuma kabla Salha wa Hammer hajatimka zake Five stars modern taarab alifanikiwa kurekodi wimbo uitwao "No discussion" ambao tayari upo katika vituo mbalimbali vya redio ukichezwa.

Lakini mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Umegundua ama umebaini kwamba wimbo huo umerekodiwa tena upya na muimbaji Kibibi Yahya katika studio za soundcrafters temeke kwa producer bora kwa sasa katika taarab nchini Mr Enrico, na hii ni baada ya Salha wa Hammer Q! kuamua kuhama bendi na kuelekea zake Five stars modern taarab.

Mtandao huu unazo nakala zote mbili za nyimbo hiyo ambayo moja imeimbwa nae Salha na ya pili imeimbwa nae Kibibi
Yahya, tunawaahidi wasomaji wetu kwamba tutaweka nyimbo hizo katika mtandao huu ili mpate kusikiliza na ku-download alafu mtatoa maoni yenu kati ya Kibibi Yahya na Salha wa Hammer ni nani ambae ameutendea haki kwa kuuimba vizuri wimbo huo? Tusubiri!.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA