PLUIJM ASEMA YANGA ITAKUWA MABINGWA WA BARA MSIMU HUU
Baada ya timu yake kuendelea kupata ushindi mfululizo katika mechi za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm, ametamba kuwa sasa njia ni nyeupe kwa kikosi chake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.
Yanga juzi ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wa mchezo huo 'Maafande' wa JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani na kufikisha pointi 40, hivyo kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm, alisema ushindi wa kila mechi huifanya timu yake kujiweka katika mazingira mazuri ya kuunyakua ubingwa wa ligi na pia kufanya vyema kwenye mashindano ya kimataifa wanayoshiriki.
Kocha huyo alisema kwamba anafurahi kuona wachezaji wake wanapambana kuhakikisha wanatimiza malengo waliyojiwekea ya kuibuka na ubingwa msimu huu.
"Njia iko wazi na ni nyeupe, tunahitaji ubingwa wa ligi na si kitu kingine, hayo ndiyo malengo tuliyojiwekea ndani ya timu," alisema kocha huyo raia wa Uholanzi anayesaidiwa na mzawa Boniface Mkwasa. Aliongeza kuwa anajua kiu ya ubingwa haiko Yanga pekee bali kwa kila timu, hivyo wanatakiwa kujipanga ili kutimiza malengo waliyojiwekea.
"Ushindani upo na tena si kwa klabu moja, najua na wao pia wanajua sisi tunautaka ubingwa, natumai mambo yatakwenda vizuri na ndiyo moja ya mikakati na mipango ya klabu, ubingwa utaleta furaha na kusahau machungu mengine," Pluijm aliongeza.
Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye mashindano ya kimataifa, wana jumla ya pointi 40 baada ya kucheza mechi 19 wakati mabingwa watetezi, Azam wanafuatia kwenye msimamo wakiwa na pointi 36 lakini wakiwa wamecheza mechi 18.
Simba ambayo ni ya tatu kwenye msimamo huo wa ligi inayoshirikisha timu 14, ina pointi 32 baada ya kucheza mechi 20 na ikiwa na rekodi nzuri ya kupata pointi nne kutoka kwa mpinzani wake Yanga msimu huu kufuatia kutoka sare mzunguko wa kwanza na ushindi wa mabao 2-0 katika raundi ya pili.
Timu tatu zinazoshika mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo ni pamoja na Polisi Morogoro yenye pointi 21 sawa na Stand United ya Shinyanga wakati Prisons ya Mbeya ndiyo inaburuza mkia kwa kuwa na pointi 17.
Ligi ya Bara wiki hii imesimama kupisha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Malawi ambayo itapigwa kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza Jumapili.