CHANONGO RUKSA KWENDA YANGA

Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini umetangaza rasmi kuachana na winga wake Haroun Chanongo ambaye alikuwa amepelekwa kwa mkopo Stand United ya Shinyanga, Chanongo anahusishwa na mipango ya kujiunga na Yanga SC ambao ni watani wa jadi wa wekundu hao wa msimbazi.

Mwenyekiti wa kamati ya kamati ya usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspoppe amesema juzi kuwa Simba haina mpango wa kumrejesha tena katika kikosi chake kiungo huyo aliyeibuliwa kutoka kikosi cha pili sambamba na nyita wengine wanaong' ara katika kikosi hicho.

Hanspoppe alisema klabu yake iko mbioni kuwarejesha nyota wake wote waliotolewa kwa mkopo isipokuwa Chanongo ambaye inadaiwa aliisaliti timu hiyo na pia amekuwa na mapenzi makubwa na Yanga, Chanongo hivi karibuni alitangazwa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya TP Mazembe ya DRC.


Pia klabu ya Yanga iko mbioni kumnasa nyota huyo ambaye pia yumo katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, wakati Chanongo akitajwa kusajiliwa na Yanga, Amri Kiemba ambaye naye alitolewa kwa mkopo Azam FC huenda akasajiliwa rasmi na timu hiyo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA