NI VITA KATI YA MZEE YUSUF NA ISHA MASHAUZI TRAVERTINE JUMAPILI

Keshokutwa jumapili ktk ukumbi wa Travertine uliopo Magomeni jijini Dsm patakuwa hapatoshi wakati bendi mahasimu za muziki wa taarabu zitakapochuana vikali kwa kiingilio cha shilingi 10, 000.

Mashauzi Classic inayoongozwa na mkurya wa kwanza kuimba taarabu mwanadada Isha Ramadhan na kundi la Jahazi Modern Taarabu chini yake mfalme Mzee Yusuf. Tayari Isha Mashauzi ameshatangaza kumgaragaza bosi wake wa zamani Mzee Yusuf na amewataka wapenzi na mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ndani ya Travertine.


Naye mfalme Mzee Yusuf ameahidi kuendeleza ufalme wake huku akidai mkubwa ni mkubwa tu, makundi hayo mawili yameanza kuwa hasimu kutokana na vinara wa makundi hayo kutambiana, Mashauzi aliwahi kufanya kazi Jahazi hivyo kuondoka kwake kumepelekea kuanzisha upinzani mkubwa


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA