CHAMA CHA WAZIRI MKUU ISRAEL CHASHINDA TENA UCHAGUZI

Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel wa chama cha Likud kilichoshinda uchaguzi mkuu wa tarehe 17 Machi 2015

Chama cha Likud cha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kimepata ushindi wa kushangaza katika uchaguzi mkuu wa Israel. Vimeripoti vyombo vya habari vya Israel.

Matokeo ya awali yalionyesha chama cha mrengo wa kushoto cha Zionist Union kupata mshitiko.


Huku kura nyingi zikiwa zimehesabiwa, Likud kinaonekana kupata viti 29 katika bunge lenye viti 120, huku chama cha Zionist Union kikiwa na viti 24.

Matokeo haya yakithibitishwa, itaonyesha kuwepo kwa serikali nyingine ya mseto itakayoongozwa na Bwana Netanyahu.
Yitzhak Herzog kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Zionist Union

Bwana Netanyahu atahitaji kuungwa mkono kutoka vyama vingine ili kuunda serikali ya mseto.

Katika hotuba kwa wafuasi wake mjini Tel Aviv baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura Jumanne, Bwana Netanyahu amesema tayari amezungumza na viongozi wa vyama vingine vyenye mrengo wa kulia kuhusu kuunda serikali mpya "bila kuchelewa".

Bwana Netanyahu amehodhi siasa za Israel kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka 20.

Kiongozi wa muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto wa Zionist Union Yitzhak Herzog amekishutumu chama tawala cha Likud kwa kudidimiza viwango vya maisha ya raia wa Israel na amekuwa akipiga kampeni dhidi ya sera za nje za Bwana Netanyahu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA