Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NGASA AIPA MKONO WA KWAHERI YANGA

Winga hatari wa Yanga na Taifa Stars, Mrisho Ngasa, amewaaga na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumpa sapoti katika kipindi chote alichokaa kwenye klabu hiyo ya Jangwani.

Ngasa, mfungaji bora wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwaka jana na mfungaji bora wa Yanga msimu uliopita, mwishoni mwa wiki alikisaidia kikosi cha wanajangwani kupata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo ya hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Ngasa alifunga mabao mawili na kupika mengine mawili, lakini muda mfupi baada ya mechi hiyo aliandika maneno kwenye ukurasa wake wa Instagram yanayoashiria kuondoka Yanga.


“Kwa heri Yanga. Nakupenda, nashukuru kwa kila kitu,” ulisomeka ukurasa wa Ngasa wa Instagram juzi jioni.

Mwandishi ilimpigia simu Ngasa jana mchana, lakini hakupokea huku uongozi wa Yanga ukiweka wazi kwamba atakuwa huru kuondoka Jangwani baada ya msimu huu.

"Kwenye ukurasa ule yale si maneno ya Ngasa, ninadhani kuna mtu ameamua kufanya hivyo. Hata hivyo, Ngasa hajasaini mkataba mpya na Yanga, hivyo yuko huru kujiunga na timu nyingine baada ya kumalizika kwa msimu huu," alisema Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano na Yanga baada ya kutafutwa kwa simu jana alasiri.

Katika mechi dhidi ya Platinum FC, Ngasa ambaye miezi miwili iliyopita aliweka wazi kutokuwa na furaha Yanga kutokana na deni la zaidi ya Sh. milioni 40 alizowalipa Simba kufanikisha kuwatumikia mabingwa hao mara 24 wa Tanzania Bara, hakushangilia mabao yote waliyofunga Jumapili dhidi ya Platinum FC.

Nyota huyo alionekana akikutanisha viganja vyake ikiwa ni ishara ya shukrani huku pia akionyesha ishara ya kulia, kilio ambacho hata hivyo, kilihusishwa na kifo cha kocha Sylivester Marsh aliyemuibua.

Katika ukurasa wake huo, Ngasa aliposti picha yake ya mechi ya juzi akilia na aliambatanisha na maneno hayo.

Mbali na Yanga, mkali huyo wa kufumania nyavu, amewahi kuzichezea timu za Kagera Sugar, Azam FC na Simba.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa