MKOLA MAN KUITANGAZA TANGA.
Staa anayechipukia kwenye kiwanda cha muziki bongo Christopher Mhenga ukipenda Mkola Man ameapa kuitangaza Tanga katika ramani ya muziki tofauti na wanamuziki wengine waliopata kutamba kupitia mkoa huo uliosifika kwa mengi.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Mkola Man amesema kuwa wanamuziki wengi waliopata kung'ara wanaotokea mkoa huo walishindwa kuitangaza vema baada ya kukimbilia jijini Dar es Salaam, lakini yeye ataendelea kuitangaza Tanga.
Kwa sasa msanii huyo anatamba na wimbo wake mpya uitwao 'Kilevi Changu' na tayari umeanza kusikika baadhi kwenye vituo vya redio, ila mikakati yake ni kuendelea kubakia jijini Tanga na kutokimbilia Dar es Salaam.
(Mkola Man wa pili kutoka kushoto, akiwa na wasanii wenzake jijini Tanga hivi karibuni)
'Unajua wanamuziki wengi waliopata kutikisa hapa nchini ambao wanatokea Tanga wameshindwa kuitangaza vema, hasa ukiangalia kundi la Wagosi wa Kaya wenyewe asili yao Tanga lakini walijikita Dar es Salaam, hivyo hivyo kwa wasanii wengine wamekimbilia Dar', alisema Mkola Man.
Baadhi ya wanamuziki waliotokea Tanga ni pamoja na Seif Shaaban Matonya, Bwana Misosi, Dan Msimamo na wengineo ambao wamehamishia makazi yao jijini Dar es Salaam, lakini staa huyo anayekuja kasi ameahidi kufanya kazi zake ndani ya Tanga ili aweze kutangaza utalii uliopo hapo.
Mkola Man na wenzake wanafanya kazi zao jijini Tanga huku yeye akiweka maskani yake Hale, mbali ya kutamba na wimbo wake mpya, Mkola Man aliwahi kutamba na kuingia kwenye Top Ten za redio mbalimbali.