Ruka hadi kwenye maudhui makuu

IVO MAPUNDA AJIPELEKA SIMBA.

KIPA aliyerejeshwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya miaka mitano, Ivo Mapunda amesema Mkataba wake na Gor Mahia ya Kenya unaisha mwezi ujao hivyo Simba SC ambao wanatafuta kipa kama wameridhishwa na uwezo wake, anawakaribisha kwa mazungumzo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya mechi ya jana baina ya Taifa Stars na timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars iliyoshinda 1-0, Ivo alisema kwamba milango iko wazi kwamba Simba SC kumfuata kwa mazungumzo.

“Ndiyo najua Simba SC wanatafuta kipa, mimi nasema kama wameridhishwa na uwezo wangu, waje tuzungumze na tukikubaliana nitawafanyia kazi nzuri,”alisema.

Ivo aliidakia Stars kwa dakika 45 kipindi cha pili jana akimpokea Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyefungwa bao hilo la Elias Maguril aliyeunganisha pasi ya Juma Luizio.

Mapema juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wanatafuta kipa atakayekwenda kuwa pamoja na makipa wazawa, Abuu Hashimu na Andrew Ntalla, kwa kuwa wana mpango wa kuachana na kipa Mganda, Abbel Dhaira.


“Niseme wazi, tunatafuta kipa. Huu ni mchakato makini sana na hatutaki kurudia kosa. Tunatafuta kipa mzawa, kwanza awe mwaminifu na mwenye uwezo mkubwa,”alisema.

Ivo alikuwa kipa namba wa Tanzania wakati wa Marcio Maximo na tangu amejiunga na St George ya Ethiopia akitokea Yanga SC, hajawahi kuitwa tena Stars hata aliporejea nyumbani kuchezea African Lyon kabla ya kwenda Gor Mahia.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe