SAKATA LA NGASA LATINGA FIFA
Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umesema unatarajia kujipanga kupeleka malalamiko yao katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ili kupinga adhabu ya kufungiwa mechi sita na kuilipa Simba Sh. milioni 45 ambayo amepewa mshambuliaji wake mpya, Mrisho Ngasa (Pichani).
Hata hivyo, Ngasa tayari ameshaanza kuitumikia adhabu hiyo na tangu Agosti 23 mwaka huu Yanga ilipowasilisha rufaa yake ya kupinga maamuzi hayo haijajibiwa chochote na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF); ambalo kanuni zake zinasema kwamba Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji ndiyo ya mwisho katika suala la usajili wa wachezaji.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema kwamba klabu yake inapinga adhabu hiyo kwa kuzingatia kanuni za FIFA za usajili ambazo zinakataza klabu kuingia mkataba na mchezaji ambaye bado hajamaliza mkataba na timu nyingine.
Mwalusako alisema kuwa kipengele 3 (f) cha FIFA kinachohusiana na Hadhi za Wachezaji kinaeleza kwamba kuna vipindi viwili vya usajili na kwa sababu hiyo, wanahoji kuwa je; Simba ilimsajil Ngasa wakati gani ilhali alikuwa bado ana mkataba na Azam?
Alisema vilevile kuwa kamati hiyo iliyomuadhibu Ngasa haikumtendea haki kwa kutomuita na kumsikiliza hali ya kuwa awali mshambuliaji huyo mwaka jana alionyesha wazi mapenzi yake kwa Yanga licha ya kuitumikia Azam wakati huo na kuna wakati klabu hiyo ilitangaza kukasirishwa na jambo hilo na kilichofuatia ni mchezaji kuhamishiwa Simba kwa mkopo.
“Ngassa hakuitwa, alinyimwa haki ya msingi ya kusikilizwa na kamati ili kuthibitisha kuhusu tuhuma za kupokea fedha kabla ya kuamua kumpa adhabu kali kama hiyo," alisema Mwalusako.
Aliongeza kwamba wanaamini Simba ilitumia mbinu ya kumrubuni na kumshawishi asaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo nje ya utaratibu wa usajili na wao wanashangaa kuona klabu hiyo (Simba) kutoadhibiwa kwa kosa hilo la kikanuni.
"Kitendo cha kumfungia Ngasa mechi sita ni kuiadhibu klabu ya Yanga kwa kosa ambalo haijahusika nalo.
Yanga imemsajili mchezaji huyu kihalali na ndiyo maana amepitishwa kuichezea timu hii msimu huu," alieleza. Aliongeza kwamba wanashangaa kuona mchezaji huyo akifungiwa kuichezea Yanga na shirikisho hilo kupitia kocha mkuu wa timu ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen, ikimuita kwa ajili ya kwenda kuitumikia nchi.