NI CHEKA AU MMAREKANI KUIBUKA MBABE LEO!
Pambano la ngumi la kimataifa kati ya bondia Francis Cheka wa Morogoro na Phil 'The Drill' Williams (Pichani) wa jimbo la Minneapolis, Minnesota nchini Marekani la kuwania mkanda unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBU) linatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Rais wa WBU, Golden Howard, alisema kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na mabondia wameshaelezwa taratibu za kuwania mkanda huo.
Howard alisema kuwa pambano hilo litasimamiwa na majaji watatu na kati ya hao wawili ni Watanzania na mmoja ametoka Afrika Kusini ambaye tayari aliwasili nchini tangu juzi.
Rais huyo aliwataka mabondia hao kuonyesha mchezo mzuri katika pambano hilo la hadhi ya juu linalotarajiwa kuvutia wadau mbalimbali wa mchezo huo wa ndani na nje ya nchi.
Cheka ambaye ana rekodi nzuri nchini baada ya kupima uzito alitamba kufanya vizuri katika pambano hilo huku akieleza kuwa anafahamu anakutana na mpinzani mwenye uzoefu wa kimataifa.
"Nimejiandaa vyema na naamini sitawaangusha Watanzania wenzangu, niko fiti kila idara," alisema Cheka.
Williams naye alitamba kwamba amekuja Tanzania kusaka ushindi na amejipanga kumpiga Cheka kwa KO.
"Nitampiga kwa KO mpinzani wangu, hatachukua muda," alisema kwa kifupi Williams ambaye muda wote alikuwa akinywa maji pamoja na matunda ya apple.
Wakati huo huo, Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC), Yasin Abdallah, alisema kuwa mpinzani wa Alphonce Mchumiatumbo kutoka Marekani, DeAndre 'Showtime' McCole hadi jana alikuwa hajawasili nchini kutokana na kutoka tiketi na hivyo sasa atapigana na bondia mwingine wa hapa nchini.
Yasin aliwataka mabondia wote kuwahi kufika ukumbini kama taratibu za mchezo huo zinavyoeleza kimataifa ili wapate muda wa kupumzika wakiwa ukumbini hapo.
"Tunatarajia kuwa na wageni wakubwa, huenda Rais (Jakaya) Kikwete na Waziri wa Michezo (Fenella Mukangara) watakuwapo, ule ushabiki wa kihuni usiwepo," aliongeza.
Mratibu wa pambano hilo, Jay Msangi, alisema kuwa maandalizi yamekamilika kama walivyopanga na wanaamini pambano hilo litaweka historia nyingine ya ngumi nchini kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Alitaja mapambano mengine ya utangulizi yatakayokuwapo leo kuwa ni la raundi 12 kuwania la kuwania ubingwa wa mkanda wa Afrika uzito wa juu wa kati (Super Middle) ambapo Mada Maugo (15-9, KO 11) aliye namba tatu kwa ubora nchini atakapopambana na Thomas Mashali (8-1, KO 5) wote wa hapa nchini huku Cosmas Cheka (8-3) atapigana na Alan Kamote (20-6, KO 12) katika pambano la raundi sita.