MGONGOLWA AIKATA MAINI YANGA KUHUSU NGASA

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa (Pichani) amesema kamati yake haikumhoji winga wa Yanga, Mrisho Ngassa ilijitosheleza na maelezo ya kimaandishi.

Ngasa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano na kutakiwa kuilipa Simba kiasi cha Sh45 milioni kufuatia kubainika kusajili mikataba ya klabu mbili kwa wakati mmoja.

Klabu yake ya Yanga imekata rufaa kupinga uamuzi huo, ambapo pamoja na mambo mengine inaona mchezaji wake hakupewa haki ya kujieleza kufuatia tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.

Lakini jana wakati Mwenyekiti, Mgongolwa akizungumza alisema kamati yake inafanya kazi na vielelezo vya maandishi, hivyo hawakuona sababu ya kumwita Ngasa.

“Kimsingi, watu wanatakiwa kufahamu, sisi kama kamati tunatumia maelezo ya maandishi ambayo ndio vithibitishoi vyetu, na kama ushahidi wa vielelezo utakuwa na upungufu ndipo tunapomwita mchezaji,” alisema Mgongolwa. Akifafanua alisema: “Kuna wachezaji wengi usajili wao umeonekana kuwa na matatizo, lakini hatukuwai kuwahoji.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA