POULSEN AENDELEA KUMBEBA JUMA KASEJA
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen
amesisitiza kuwa kipa na nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja (Pichani) bado yuko
katika kiwango cha juu na ndiye chaguo lake la kwanza licha ya kuachwa
na klabu yake ya Simba katika kikosi chao cha msimu ujao wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara.
Poulsen aliyasema hayo jana jijini Mwanza wakati Stars ikikaribia kwenda Uganda kujiandaa kwa mechi yao ya keshokutwa dhidi ya wenyeji (The Cranes) kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Poulsen alisema kuwa kiwango cha Kaseja kimekuwa kikiongezeka kadri siku zinavyokwenda na hiyo inatokana na uzoefu alio nao katika umri wake wa sasa wa miaka 29.
Kocha huyo aliongeza kuwa kwa nafasi ya kipa, umri wa Kaseja ndiyo mzuri zaidi kwani mchezaji wa kiwango cha juu kama yeye anakuwa tayari ameshapata uzoefu wa kutosha kutokana na mechi nyingi alizocheza katika ligi mashindano ya kimataifa.
"Angalia kiwango chake... bado ni cha juu na siku hadi siku anazidi kuimarika. Angalia alivyofanya vizuri tulipocheza dhidi ya timu kubwa kama Cameroon. Kwa ujumla timu nzima inajengeka na yeye uzoefu wake ni muhimu zaidi," alisema kocha huyo raia wa Denmark.
Hivi karibuni, uongozi wa Simba ulitangaza kumuacha Kaseja kwa kutompa mkataba mwingine wa kuidakia timu hiyo aliyotumikia kwa takriban muongo mmoja.
Katika hatua nyingine, Poulsen alikiri kwamba kutoroka kambini kwa kiungo Mwinyi Kazimoto wa Simba kumemuharibia mipango yake kwani sasa watalazimika kuziba nafasi yake kwa usahihi na pia wanapaswa kupangua safu ya ulinzi baada ya kuondoka kwa beki Shomari Kapombe anayetarajiwa kufanyiwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Uholanzi.
"Siwezi kusema tutatumia mfumo gani (dhidi ya Uganda) kwa sababu tutakuwa tunatoa siri kwa wapinzani wetu. Ila naamini tutafanya vizuri katika mechi hii ya ugenini," aliongeza, huku akiliacha suala la kutoroka Kazimoto kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Stars ilifungwa goli 1-0 katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Uganda iliyochezwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa na hivyo watalazimika kujibu mapigo kwa kushinda keshokutwa kwa walau 2-0 ili wasonge mbele katika michuano ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Afrika Kusini.