KIMEELEWEKA, HATIMAYE FABREGAS KUNUKIA MAN UNITED
KIUNGO Cesc Fabregas amewaambia rafiki zake England kwamba anataka kuondoka Barcelona kuhamia Manchester United.
Kiungo
huyo wa Hispania kwa sasa anagombewa na United na Barcelona, na
mabingwa hao wa Ligi Kuu y England wamekwishatoa ofa ya Pauni Milioni
30.
Kocha
wa United, David Moyes aliwaambia Waandishi wa Habari nchini Japan jana
kwamba mpango wa klabu hizo kufanya biashara ya nyota huyo wa zamani wa
Arsenal unaendelea na ofa nyingine itatolewa.
Lakini
habari kwamba Fabregas amewaambia rafiki zake England kwamba anataka
kuondoka Nou Camp hatimaye zinaweza kuwapa faraja United.
Inafahamika
Fabregas anavutiwa na ahadi ya kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi
cha kwanza United na yuko tayari kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani
wa Arsenal, mshambuliaji wa United, Robin van Persie.
Fabregas
pia anaamini anaweza kutwaa taji la England na United kuunganisha na
lile moja aliloshinda Hispania la La Liga msimu uliopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameshinda taji la FA na Ngao ya Jamii pekee katika kipindi chake cha kuichezea Arsenal.
Barcelona wameendelea kutia kauzibe wakiiambia United kwamba, kiungo wao hawamuuzi."Vidic,
Nani nad Antonio Valencia wote wanacheza nao. Wayne Rooney pia
anakimbia na katika kiwango ambacho tunafikiri atakuwa fiti. Atapiga
hatua wiki hii,".
Muungano wawezakana: Uwezekano wa Robin van Persie kuungana na Fabregas tena wawezekana
Muonekano mpya United: David Moyes na Steve Round sasa ni makocha Old Trafford
Watarudisha enzi: Van Persie na Fabregas walifanya kazi pamoja kwa mafanikio Arsenal
Kikosi cha vipaji: Fabregas pia anaweza kuvutiwa na hamu ya kushinda katika soka ya England
Iwapo Fabregas ataamua kuomba kuondoka, mambo yanaweza kubadilika.
United
inatarajiwa kucheza mechi yake ya nne katika ziara yake ya kujiandaa na
msimu, leo ikimenyana na Cerezo Osaka saa 5:00 asubuhi za Uingereza.
Van
Persie anatarajiwa kucheza sehemu kidogo baada ya kupata ahueni ya
maumivu yake, wakati Moyes pia amesema kwamba Nahodha wake, Nemanja
Vidic — ambaye pia amekuwa majeruhi ameanza kucheza soka ya ushindani
nyumbani England.
Moyes alisema: "Kunakuwa kuna mechi za mazoezi siku nyingine Carrington.
Jezi mpya: Kuna mabadiliko mengi United tangu mwishoni mwa msimu
Treni ya umeme: Kikosi cha United kimekuwa kikisafiri kwa staili ya aina yake Japan