Machapisho

Mzize uso kwa uso na Skudu Makudubela Afrika Kusini

Picha
Winga wa zamani wa Yanga SC, Skudu Makudubela amekutana na Mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize ambaye yupo Afrika Kusini kupatiwa matibabu ya mguu. . Skudu alimpelekea Mzize ujumbe wa kumtakia heri ya kupona haraka kupitia Ki-memo alichobeba.

Nsajigwa awaaga Transit Camp

Picha
Leo nimewaaga sio tu kama wafanyakazi wenzangu, bali kama familia yangu ya pili. Kipindi tulichokuwa pamoja,kilikuwa zaidi ya mpira , kilikuwa ni safari ya upendo, mshikamano, kujifunza na kukua pamoja. Nimejifunza mengi kupitia viongozi wetu, wachezaji wangu na mashabiki waliotuunga mkono kila hatua katika Kutafuta ushindi uwanjani, Ushirikiano wenu umeacha alama kubwa moyoni mwangu. Leo naanza safari mpya katika timu ya daraja la juu, lakini moyo wangu utaendelea kubeba kumbukumbu na heshima kubwa kwenu. Nawashukuru sana kwa sapoti, ushirikiano na urafiki wa kweli. Nawatakia mafanikio makubwa zaidi, malengo yenu yatimie, tuendelee kuwa na furaha, umoja na mshikamano ndani na nje ya uwanja. Asanteni sana Viongozi, Wachezaji na Mashabiki wa Transit Camp. Mtabaki kuwa sehemu ya historia yangu milele. Ikumbukwe Nsajigwa anaenda kuanza kazi ya kuwa kocha mpya wa timu ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu bara na anapewa jukumu kubwa la kuhakikisha timu hiyo inasalia Ligi Kuu. Kwa upen...

Mkwasa ampa tano Seleman Kitunda

Picha
NA Na Mwandishi Wetu KOCHA na mchezaji wa zamani wa timu za Yanga SC timu ya taifa, na Taifa Stars. Charles Boniface Mkwasa "Master" amemsifu vilivyo kocha mkuu wa timu ya Cosmopolitan. Seleman Kitunda "Guardiola" kwa kuweza kuimudu Yanga walipocheza nao na kuruhusu idadi ndogo ya mabao ya kufungwa tofauti na makocha wakubwa na wazoefu Ahmad Ally wa JKT Tanzania na Salum Mayanga wa Mashujaa FC. Akizungumza na Mambo Uwanjani Blog. Mkwasa amemsifu Kitunda akidai ni kocha mzuri na timu yake ilizidiwa maenen machache na Yanga ingawa aliweza kuwabana Yanga ma kufungwa idadi ya ndogo tofauti na wenzake. Katika mchezo huo wa kombe la CRDB , Yanga iliifunga Cosmopolitan mabao 2-0 Mkwasa ameongeza kuwa Kitunda aliifanya timu yake kushambulia kwa nidhamu. lakini Ahmad Ally wa JKT Tanzania timu yake imekubali kichapo kikubwa toka kwa Yanga cha mabao 5-0 na Salum Mayanga wa Mashujaa FC alikubali kichapo cha mabao 6-0 kabla ya timu hiyo haijamtupia virago vyake. Kwa kifupi Mkwas...

Singida Black Stars yampiga stop Aucho

Picha
Klabu ya Singida Black Stars imemsimamisha kazi miezi mitatu kiungo wake Khalid Aucho raia wa Uganda kwa utovu wa nidhamu na utoro kazini, uamuzi uliotolewa leo Februari 27, 2026 na Kamati ya Nidhamu ya klabu hiyo. Katika hatua nyingine klabu hiyo imemsimamisha kazi miezi mitatu golikipa Amas Obasogie kupisha uchunguzi wa tuhuma za upangaji wa matokeo. Singida Black Stars imewakumbusha wachezaji na watumishi wake wote kuzingatia nidhamu, uwajibikaji na heshima kwa klabu.

Simba wapo tayari kuwavaa Yanga Zanzibar

Picha
Wachezaji wa timu ya Simba SC wakiwa Zanzibar tayari kwa ajili ya mtanange wao dhidi ya Yanga SC siku ya Jumapili katika uwanja wa New Amaan Stadium, mchezo wa Ligi Kuu bara. Wachezaji wa Simba SC wakiwasili.

Yanga yaipashia Simba Zanzibar

Picha
Kikosi cha Yanga SC kimefanya mazoezi yake ya kwanza visiwani Zanzibar ikijiandaa na mchezo wao dhidi ya Simba SC. . Pacome Zouzoua naye alikuwepo.

Pacome yupo tayari kwa dabi, akwea boti kuwafuata Simba

Picha
Kiungo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ivory Coast na Klabu ya Yanga SC, Pacome Pedoh Zouzoua amesafiri na Kikosi cha Yanga kuelekea visiwani Zanzibar tayari kwa mchezo wa Derby dhidi ya Simba SC. . Pacome ameshapona na yupo tayari kuwakabili Simba, uwepo wa Pacome unazidi kuwachanganya mashabiki wa Simba ambao bado hawana furaha anapokuwepo mchezaji huyo kwenye kikosi cha Yanga.