Mkwasa ampa tano Seleman Kitunda
NA Na Mwandishi Wetu
KOCHA na mchezaji wa zamani wa timu za Yanga SC timu ya taifa, na Taifa Stars. Charles Boniface Mkwasa "Master" amemsifu vilivyo kocha mkuu wa timu ya Cosmopolitan. Seleman Kitunda "Guardiola" kwa kuweza kuimudu Yanga walipocheza nao na kuruhusu idadi ndogo ya mabao ya kufungwa tofauti na makocha wakubwa na wazoefu Ahmad Ally wa JKT Tanzania na Salum Mayanga wa Mashujaa FC.
Akizungumza na Mambo Uwanjani Blog. Mkwasa amemsifu Kitunda akidai ni kocha mzuri na timu yake ilizidiwa maenen machache na Yanga ingawa aliweza kuwabana Yanga ma kufungwa idadi ya ndogo tofauti na wenzake.
Katika mchezo huo wa kombe la CRDB , Yanga iliifunga Cosmopolitan mabao 2-0 Mkwasa ameongeza kuwa Kitunda aliifanya timu yake kushambulia kwa nidhamu. lakini Ahmad Ally wa JKT Tanzania timu yake imekubali kichapo kikubwa toka kwa Yanga cha mabao 5-0 na Salum Mayanga wa Mashujaa FC alikubali kichapo cha mabao 6-0 kabla ya timu hiyo haijamtupia virago vyake.
Kwa kifupi Mkwasa anadai kwamba Kitunda ameonyesha uwezo mkubwa na anaweza kuisaidia Cosmopolitan kupanda Championship endapo watacheza kwa nidhamu ile ile walipocheza na Yanga SC.
Mkwasa pia amewahi kuzinoa timu za Ruvu Shooting, Tanzania Prisons na nyinginezo.

