Nsajigwa awaaga Transit Camp

Leo nimewaaga sio tu kama wafanyakazi wenzangu, bali kama familia yangu ya pili. Kipindi tulichokuwa pamoja,kilikuwa zaidi ya mpira , kilikuwa ni safari ya upendo, mshikamano, kujifunza na kukua pamoja.

Nimejifunza mengi kupitia viongozi wetu, wachezaji wangu na mashabiki waliotuunga mkono kila hatua katika Kutafuta ushindi uwanjani, Ushirikiano wenu umeacha alama kubwa moyoni mwangu.

Leo naanza safari mpya katika timu ya daraja la juu, lakini moyo wangu utaendelea kubeba kumbukumbu na heshima kubwa kwenu. Nawashukuru sana kwa sapoti, ushirikiano na urafiki wa kweli.

Nawatakia mafanikio makubwa zaidi, malengo yenu yatimie, tuendelee kuwa na furaha, umoja na mshikamano ndani na nje ya uwanja.

Asanteni sana Viongozi, Wachezaji na Mashabiki wa Transit Camp.
Mtabaki kuwa sehemu ya historia yangu milele.


Ikumbukwe Nsajigwa anaenda kuanza kazi ya kuwa kocha mpya wa timu ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu bara na anapewa jukumu kubwa la kuhakikisha timu hiyo inasalia Ligi Kuu.
Kwa upendo na heshima
Coach Nsajigwa Shadrack
Fuso14


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI