Machapisho

Clara Luvanga awashangaa wanaume kutomtongoza

Picha
Clara Luvanga asema anashindwa kuwaelewa wanaume kwa kutomtongoza! Mchezaji wa Al-Nassr na Twiga Stars, Clara Luvanga amesema kuwa hatumiwi meseji na wanaume huku akitaja 'UOGA' kama sababu kuu miongoni mwa wanaume.

Mamelodi yashikwa na Pyramids

Picha
WENYEJI, Mamelodi Sundowns wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Pyramids FC ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, Afrika Kusini. Mabao yote yalifungwa na viungo – Mbrazil Lucas Ribeiro Costa akianza kuifungia Mamelodi Sundowns dakika ya 54, kabla ya Mmorroco Walid El Karti kuisawazishia Pyramids FC dakika ya 90’+4.

Kocha RSB Berkane aihofia Simba

Picha
Kocha mkuu wa RSB Berkane Mouain Chaaban amesema wana furaha sana kucheza mechi hii dhidi ya Simba, lakini amedai mechi itakuwa ngumu kwakuwa timu hiyo inacheza nyumbani kwake. "Tuna furaha kucheza mechi hii dhidi ya Simba japo tunafahamu kuwa haitokuwa mechi rahisi kwa timu zote mbili" maneno ya Kocha Mouain Chaaban wa RS Berkane akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) mchezo wa mkondo wa pili. Ni Simba SC dhidi ya RS Berkane Mechi ni kesho Mei 25 saa 10:00 jioni itakuwa live Azam Tv

Fadlu awapiga mkwara Berkane, asema awaogopi

Picha
"Sisi tunahitaji Mwamuzi Ambae Atausimamia Mchezo kwenye njia sahihi hasa kwenye upotevu wa muda, mwamuzi ajitahidi tucheze angalau dakika 60, sisi Simba tunahitaji mwamuzi atakaekuwa imara kwenye kutunza muda kwa wachezaji ambao watakuwa wanaanguka makusudi uwanjani." "Ndio Berkane wanahitaji kushinda na tayari wapo mbele kwa mabao 2-0 dhidi yetu na watacheza taratibu hilo ni kawaida ila sio Kipa amedaka mpira halafu adondoke chini hivyo mwamuzi anapaswa kuwa imara ikitokea mchezaji ameumia asimamishe muda halafu baadae aendelee na hata kwenye kutoka na kuingia, kwenye kutibiwa pia hivyo tunahitaji mwamuzi awe imara." "RS Berkane ni timu ya daraja la juu lakini bado hawajakutana na hasira ya Simba Sports Club ikiwa kwenye ubora na uwezo wake kamili, mchezo wa kwanza kule Morocco tuliuchukulia kama somo kwetu na sasa tupo tayari kwa mchezo." Fadlu Davids Head Coach Simba SC.

Mrithi wa Diarra Yanga huyu hapa

Picha
Young Africans SC itamrejesha Goalkeeper wao Amas Obasogie ambaye walimtoa kwa mkopo kwenda Singida Black Stars, Amas Obasogie ni miongoni mwa wachezaji waliobadirisha uraia na kuwa watanzania.

Ibraa aachana rasmi na Harmonize

Picha
Rasmi sasa Ibraa amemalizana na lebo aliyokuwa akifanya nayo kazi Konde Music Worldwide baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati yake,lebo hiyo na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Makubaliano hayo yamesainiwa mbele ya Katibu Mtendaji wa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, Ibraah aliambatana na mshauri wake wa biashara, Bw. Msigwa na upande wa Konde Gang ukiwakilishwa na wakili wao, Bi. Sandra. Kupitia makubaliano hayo, Ibraah ameruhusiwa kuendelea na kazi zake za muziki bila masharti yoyote kutoka kwa lebo hiyo. Hatua hii inatoa nafasi kwa msanii huyo kujiendeleza zaidi kisanaa kwa uhuru na ubunifu wake binafsi.

Uongozi Simba wazuru kaburl la Mzee Rukhsa

Picha
UONGOZI wa Simba SC leo umezuru katika kaburi la Hayati Ali Hassan Mwinyi, Rais wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Kijiji cha Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja Wilaya ya Kaskazini B, Zanzibar na kumuombea dua aendelee kupumzika kwa Amani. Hiyo ni moja ya matukio ya kijamii kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RSB Berkane Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.