BARCELONA,MAN U ZATUPWA NJE ULAYA
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia moja ya magoli yao dhidi ya Manchester United Matumaini ya timu ya Manchester United kufanya maajabu katika ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA yaliyeyuka jana usiku wa Jumatano baada ya kupokea kipigo kutoka kwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Bayern Munich ya Ujerumani cha magoli 3-1. Hayo yalikuwa ni matokeo ya mchezo wa marudiano baada ya mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford, timu hizo kutoka sare ya magoli 1-1.