Yanga yatoa tamko kuhusu Mwenda


Klabu ya Yanga imekanusha shutuma kwamba imewahi kumtuhumu mchezaji wake Israel Patrick Mwenda kwa “Kuuza” mechi na haijawahi hata kumuandikia barua ya kumsimamisha kazi.

Yanga SC wanasema mchezaji ni MTORO kazini na hajulikani alipo na wamekuwa wakimuandikia barua za kutaka kujua alipo na kwanini hafiki kazini, lakini mchezaji hajawahi kujibu na wala hajataka kuripoti kazini.

Hali hii imeifanya klabu kutomuingizia mshahara wake kwakuwa ni mtoro kazini na hajulikani alipo. Inasemekena mchezaji aliondoka kambini kwa kuandika barua ambayo Bin Kazumari imeiona ikiwa na tarehe 03/07/2026 na kichwa cha habari UAMUZI WANGU WA KUJIWEKA PEMBENI. Kwenye barua hiyo mchezaji alisema amejithamini na kuona kwamba “uamuzi huo ulihitaji ujasiri mkubwa, lakini niliuchukulia kama sehemu ya uwajibikaji wangu ishara ya kuheshimu malengo ya pamoja ya timu”.

Yanga SC inamtambua Israel kama mchezaji wake mwenye mkataba lakini ametoweka bila taarifa “Absent Without Leave - AWOL” kwenye kituo cha kazi.

Katika hali hiyo Yanga SC wanashindwa kumlipa mtu ambaye hayuko kazini na hajulikani alipo. Mchezaji anajiweka kwenye hatari ya kukiuka vipengele vya kisheria kwenye mkataba wake. Kwa namna hiyo basi mchezaji anawajibika kurudi kazini katika namna alivyoondoka ndiyo maana klabu imeacha kumuingizia malipo yake.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI