Yanga yatambulisha beki wa kati mpya
Klabu ya Yanga SC imemtambulisha beki wa kati, Oumar Farouk Komara kama mchezaji mpya klabuni hapo baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Golden Arrows ya Nchini Afrika Kusini.
Komara 25, raia wa Ivory Coast ambaye pia ana uwezo wa kucheza kama Kiungo Mkabaji tayari yupo Geita na Kikosi cha Yanga na ujio wake unalenga kuongeza kuimarisha zaidi safu ya ulinzi na viungo wa Yanga kuelekea msimu mpya wa mashindano.
