Yanga wametoa burudani ya mabao
Na Hans Raphael
Yanga leo wametoa burudani ya mabao ya aina yake, Bao Yakideo na ufundi binafsi.
Maxi Nzengeli: Bao la pili lilikuwa Golazo la kiwango cha juu kabisa!
Mudathir Yahya ameendelea kuonyesha ukomavu kwenye umaliziaji, na kwanini ni mchezaji muhimu akiwa uwanjani.
Albert Kangwanda: Kwenye kipindi cha kwanza, alionyesha ukali kwa kubadili half-chance kuwa bao kamili akiwa ndani ya kisanduku.
Mohamed Hussein, Goli la leo karudia alichofanya kipindi alivyokuwa Simba SC, kwenye mechi ya kimataifa.
Takwimu za Kipindi cha Kwanza: Mchezo ulikuwa upande mmoja zaidi (flat performance kutoka kwa Coastal Union).
Yanga walitawala kila idara: Mpira wa Miguu (Possession): Yanga 73% vs Coastal Union 27%
Mashuti: Yanga walipiga 15 (7 zikiwa on target) na kupata mabao 2.
Coastal Union: Takwimu zote muhimu za mashambulizi zilisoma 0.
Bila umaridadi na uokoaji wa kipa Chuma Ramadhan Mgeni, coastal wangeweza kupata msiba mkubwa zaidi.
Mbinu za Low Block Hazisaidii: Kwa timu za daraja la chini au za katikati, kuingia na mbinu ya kukaba tu ndani na nje ya box (low block) dhidi ya Yanga ni kujitafutia matatizo.
Yanga wana kila aina ya silaha ya kuvunja ukuta. Subira na uthubutu wa kushambulia ndio njia pekee ya kupata matokeo kwenye soka.
Bado Coastal walionyesha mfano pale jaribio lao moja lilipozaa faulo na Gradi Kiala akafunga.
Uimara wa Timu na Wachezaji Basi
Hossaine Zakouani: Anaendelea kuonyesha kiwango bora na chenye muendelezo kwenye winga zite mbili.
Abdulnassir Mohamed “Casemiro”: Anazidi kuimarika na kuaminika kikamilifu na Kocha Manqoba Mngqithi.
Mfumo wa FVS (Football Video Support) utaendelea kuwagharimu wachezaji wasio na nidhamu ya mchezo.
Geofrey Manyasi hakuwa na sababu ya kumfanyia foul Duke Abuya na kuingia kwenye mtego wa kadi nyekundu, ingawa migongano ni sehemu ya mchezo (part of the game).
