Yanga itakutana na Gaborone United

Wawakilishi wa Tanzania katika CAF Champions League, Young Africans SC, wamepangwa dhidi ya Gaborone United ya Botswana katika raundi ya kwanza ya hatua ya awali ya michuano hiyo.

Yanga itahitaji kupata matokeo mazuri katika michezo hiyo ili kusonga mbele na kuendelea na safari ya kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya CAF Champions League.

Iwapo Yanga itafanikiwa kuiondoa Gaborone United, hatua inayofuata itawakutanisha na mshindi kati ya CFFA ya Madagascar na Lijabatho FC ya Lesotho.

Hivyo, safari ya Yanga kuelekea Group Stage ya CAF Champions League inaanza rasmi, huku klabu hiyo ikiwa na lengo la kuendelea kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa la juu la soka la Afrika.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI