Yanga haikamatiki, yailalua Coastal 4-1
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC usiku huu imepata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo Yanga insongoza ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 6, Yanga ilitangulia kupata bao kupitia kwa Albert Kangwanda na kufuatia na Maxi Nzengeli.
Kikosi hicho cha Yanga kinachonolewa na Manqoba raia wa Afrika Kusini, kiliandika bao tatu lilifungwa na Mudathir Yahya, Coastal Union walipata bao la kufutia machozi likifungwa na Gradi Kiala.
Yanga waliendeleza kulishambulia goli la Coastal na kupata bao la nne likiwekwa wavuni na Mohamed Hussein Zimbwe Jr .


