TFF yataka Yanga iilipe Simba kisa usajili wa Sele
Selemani Mwalimu ukiingia kwenye mfumo wa Usajili wa FIFA Connect anasoma kuwa ni mchezaji wa Yanga SC na si kweli Simba SC haijamuachia kwenye mfumo japo iliweka pingamizi TFF Kutaka ilipwe gharama ilizotumia wakati wanapambana kumsajili tena kwa mkopo.
Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo ni kuwa pingamizi la Simba Sports Club ilikuwa ni kutaka kuzuia Usajili wa Sele Gomez wakitaka kulipwa kwanza pesa zao walizotumia wakati wanapambana kumsajili.
Issue ilikuwa siku ya mwisho wa Usajili Simba SC walikuwa wanakataa ombi la kumuachia Selemani Mwalimu ila Yanga SC baada ya kuonesha ushahidi na makubaliano kati ya Yanga SC na Wydad Casablanca kimkataba ndipo TFF wakaruhusu usajili wa Selemani Mwalimu kwenye mfumo wa usajili wa FIFA Connect.
Kesi ipo kati ya Simba SC na Selemani Mwalimu, Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo Selemani Mwalimu hakuwa amelipwa fedha za usajili na Simba SC na fedha ambazo zinaweza kuwa anadaiwa ni tiketi ya ndege ya kutoka Morocco Kuja Tanzania.
Selemani Mwalimu ni mchezaji wa Yanga SC ambae anasomeka kwenye mfumo na anayo Leseni ya kucheza Ligi Kuu ya NBC.
