Simba yaendeleza ilipoishia
Wekundu wa Msimbazi au Simba SC jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba Bukoba mkoani Kagera.
Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na beki wa kati Ismail Toure raia wa Ivory Coast na baadaye mshambuliaji Elie Mpanzu raia wa DR Congo.
Ushindi huo ni mwanzo mzuri wa Ligi Kuu bara ikipata ushindi ugenini na kufikisha alama 3 ikishika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya Singida Black Stars inayongoza na Yanga.
