Simba Queens yatupwa nje CECAFA

Simba Queens imeondolewa katika mashindano ya CECAFA yanayoendelea Kigali, Rwanda, baada ya kushika nafasi ya pili Kundi C ikiwa na pointi tatu.

Timu hiyo ilishinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja, hivyo kushindwa kufuzu hatua ya nusu fainali.

Kenya Police Bullets ya Kenya imeongoza kundi hilo kwa pointi sita baada ya kuichapa Top Girls Academy ya Burundi mabao 3-1 na kutinga nusu fainali.

Kwa Simba Queens, matokeo hayo ni pigo katika harakati za kurejesha taji linaloshikiliwa na JKT Queens ya Tanzania. Timu hiyo imeendelea kukosa mafanikio makubwa katika miaka ya hivi karibuni.

Baada ya kufika nusu fainali mwaka 2022, ilishiriki tena mwaka 2024 na kumaliza nafasi ya nne. Matokeo ya mwaka huu yanaongeza changamoto kwa Simba Queens katika kurejesha ubabe wake kwenye soka la wanawake Afrika Mashariki na
‎kati.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI