Sijamkatia tamaa Doumbia- Barker
Aliwafunga Singida pale Rwanda CECAFA Kagame cup . Nitampa nafasi mapema aweze kunionyesha kwamba anaweza kufanya hivyo tena.
Sijawahi kuwa wa kwanza Wala wa mwisho kuhusu kuamini maendeleo ya mchezo always nachagua nyakati sahihi kuweza kutafakari,kung'amua na kufanya hitimisho kwa mchezaji kwa sababu mpira wa miguu ni process.
Ibrahim Doumbia Ni mshambuliaji ambae alikotoka alikuwa daraja la juu sana Wala sio mchezaji mbovu na anaweza kuipa Simba SC Mabao 10+ kwa msimu.
Kinachotokea sasa ni kujaribu kumuondoa kwenye zile process za kukaa sawa hasa kiakili na kuzoea mazingira mapya. Wanasimba ndio watu wa kwanza wanaotakiwa kumuamini na kumpa moyo.
Kama ilivyo kauli NGUVU MOJA basi iende hadi kuwalinda Wachezaji weru hawa Nimeangalia washambuliaji wa wapinzani yule Shalulile na Hata wengine nao wanastruggle ila mashabiki wanawalinda kama Yai na husikii kelele za kuwakatisha tamaa.
Nimemuangalia mshambuliaji mpya wa Azam FC pia ni yaleyale ila timu yake imechagua kumlinda na anafanya kazi yake bila presha na wala halazimishwi kufunga goli bali kucheza.
Nakataa kuamini Doumbia hatamudu mazingira ya Tanzania. Kuna siku atawasuprise sana mtatamani mfiche sura zenu kwa aibu. Mimi kama kocha nimechagua kumuamini.
