Ronaldo aweka wazi ataacha soka mwaka huu
Cristiano Ronaldo ametoa kauli inayoweza kuwa ishara kubwa ya mwisho wa safari yake ya soka, akisema mwaka 2026 huenda ukawa mwaka wake wa mwisho kucheza soka la kulipwa.
Akizungumza katika mahojiano na jarida la Vogue, nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 amesema:
“Huenda huu ukawa mwaka wangu wa mwisho katika soka. Nataka kuacha urithi wa ajabu. Tayari nina mipango yote ya maisha yangu ya baadaye.”
Ronaldo amesema tayari ana picha kamili ya maisha yake baada ya soka, akitarajia kutumia muda zaidi kusafiri, kuwa na familia yake na kufurahia michezo mingine kama padel.
Kauli hiyo imezua gumzo kubwa duniani, huku Ronaldo akiwa bado anaendelea kuichezea Al-Nassr na akiwa katika harakati za kufikia rekodi ya mabao 1,000 katika maisha yake ya soka.
