Patrick Vieira awa kocha mkuu Senegal
Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) limemtangaza rasmi Patrick Vieira kuwa kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya Senegal
Vieira, ambaye ni gwiji wa soka la kimataifa na aliyekuwa akiichezea timu ya taifa Ufaransa, alizaliwa jijini Dakar, Senegal.
Uteuzi huo unamfanya Vieira kurejea nchini alikozaliwa akiwa na jukumu la kuiongoza timu ya taifa ya Senegal.
Patrick amesaini mkataba wa miaka minne akichukua nafasi ya Pape Thiaw aliyeondoka mwezi uliopita.
