Mayele aibukia Al Ahli Tripoli
Mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Fiston Kalala Mayele, amejiunga rasmi na klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya akitokea Pyramids FC ya Misri kama mchezaji huru.
Mayele amesaini mkataba wa miaka miwili, utakaomuweka klabuni hapo hadi Juni 2028.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyanzo mbalimbali vya michezo, thamani ya jumla ya kifurushi cha mkataba wake inakadiriwa kufikia Dola Milioni 5 kwa miaka miwili.
Mshahara wa milioni 550 kwa mwezi pale Al Ahly Tripoli SC ambao ukiugawanya unapata around 19.7 m kwa siku
Fiston Kalala Mayele amegonga jackpot baada ya kipaji na juhudi zake,19.7m kwa siku pungufu ya 1.3m mshahara wa mwezi aliokuwa akipokea Young Africans SC (21m monthly)
