Manqoba amuhofia Mgunda

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Manqoba Mngqithi ameweka wazi kuwa anaamini kuwa Namungo watacheza kwa kujihami zaidi na kujiamini na amekiri kuwa Namungo wana Kocha mzuri sana Juma Mgunda.

"Ninaamini Namungo watakuja kwa kujiamini na kujihami kwa wakati huo huo, najua wana kocha mzuri sana na namjua tangu akifundisha timu ya Taifa, Hivyo nasisi tutatumia Ubora wetu na tutatengeneza nafasi zetu ili kushinda mechi"

Aidha kocha huyo ameongeza kuwa hawajapata muda mzuri wa kujiandaa na Mechi dhidi ya Namungo.

"Kwakweli hatujapata muda mrefu wa kujiandaa dhidi ya Namungo lakini kwa namna tulivyojipanga tangu mchezo wa Derby naamini tutakuwa kwenye mfumo wetu ule ule na Nina amini tutapata Matokeo mazuri"

-Manqoba Mngqithi (Kocha wa klabu ya Yanga kupelekea mchezo wa Ligi kuu ya NBC hapo kesho dhidi ya Namungo FC).


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI