Manara afichua siri Simba kumkosa Feitoto

Aliyewahi kuwa Msemaji wa Simba SC, Haji Manara, amefichua siri iliyopo nyuma ya pazia kuhusu Mnyama kukwama kumpata kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto'.

Manara ameeleza kuwa Wekundu wa Msimbazi walikuwa tayari kutoa kitita cha shilingi bilioni 4 za Kitanzania kwa fedha taslimu (kesh) usiku wa manane ili kukamilisha usajili huo, lakini uongozi wa Azam FC ulikataa kupokea fedha hizo na kuzuia mpango huo kukamilika.

​Akimnukuu Haji Manara kuhusu mchakato huo wa usiku wa manane na sababu za Azam FC kugoma kuingia kwenye makubaliano hayo, alisema:

​"Simba walikuwa na bilioni nne kesh kwa ajili ya kulipa Azam. Azam wakawaambia bilioni nne unazilipaje kesh? Cha kwanza too late, walichelewa yaani mpaka wamekusanya zile... mpaka ikafika hatua tajiri akasema sitaki, sitaki, sitaki!"

​Manara amebainisha kuwa mbali na utata wa kufanya muamala mkubwa wa fedha taslimu usiku wa manane, sababu nyingine kubwa ilikuwa ni Simba kuchelewa kuchanga karata zao mapema kwenye usajili huo. Kushindwa kwa dili hilo kumezua mjadala mzito miongoni mwa wadau wa soka nchini kuhusu namna klabu zinavyoendesha michakato ya usajili wa wachezaji wakubwa.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI