Simba yasimama kwa muda

Klabu ya Simba imetangaza kusimamisha kwa muda masuala yote yaliyokuwa yakiendelea kuhusu Baraza la Wadhamini, kufuatia uamuzi uliofikiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika Agosti 3, 2026.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Agosti 4, 2026 Bodi imeeleza kuwa imeamua kusimamisha matukio yote yaliyotokea awali kuhusiana na Baraza la Wadhamini hadi itakapotolewa taarifa nyingine.

Katika kipindi hicho, Bodi imesema itaelekeza nguvu zake katika masuala muhimu yanayohusu klabu, ikiwemo mchakato wa usajili wa Wachezaji, maandalizi ya Simba Day, mchezo wa Ngao ya Jamii pamoja na maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu ujao.

Aidha, Bodi imewasihi Wanachama na wapenzi wa Simba kuendelea kuiunga mkono klabu hiyo ili kuhakikisha inapata mafanikio makubwa katika msimu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Taarifa hiyo imesainiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Murtaza Mangungu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI