Kigwangala aliamsha tena Simba

Aliyekuwa Waziri na Mwanachama wa Simba SC, Dr. Hamisi Kigwangalla, ameibua mtafaruku mpya Msimbazi baada ya kuweka wazi nia yake ya kuvunja kile alichokiita "utawala wa mtu mmoja".

Huku akitangaza kuwa yuko tayari kuweka fedha taslimu (cash) mezani kununua hisa za mwekezaji mkuu wa sasa, Mohammed 'Mo' Dewji.

Kigwangalla ameyasema hayo huku akijibu shinikizo la baadhi ya wanasimba wanaomtaka agombee nafasi ya Uwenyekiti wa Simba SC kwenye uchaguzi ujao.

Sina Hamu na Siasa za Mpira, Tatizo ni Mfumo"

Akieleza sababu za kukataa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Uwenyekiti kwa sasa, Dr. Kigwangalla amebainisha kuwa tatizo la Simba silo uongozi wa mtu mmoja, bali ni muundo mbovu wa uendeshaji (governance) na umiliki wa klabu (ownership).

"Kwanza, sijioni nikijikita kwenye siasa za mpira wa miguu wa klabu kubwa kama Simba. Pili, naamini tatizo la Simba si mtu mmoja. Tatizo kubwa ni mfumo wa uongozi na umiliki," alisema Kigwangalla.

Mpango wa Kuondoa 'Veto Power' ya Mo Dewji: 👇🏼

Kigwangalla amesisitiza kuwa si afya kwa klabu kubwa kama Simba kuendelea kumilikiwa kwa 49% na mwekezaji mmoja pekee, kwani jambo hilo linampa nguvu kubwa ya maamuzi (veto power) na kuondoa uwajibikaji wa kweli kwa Bodi na Wanachama wanaomiliki 51%.

Ili kuleta mageuzi ya kweli, amependekeza hisa hizo 49% zigawanywe kwa wawekezaji watatu hadi watano:

Mo Dewji (Mwekezaji wa Sasa): Abakiwe na 15% – 20%.

Mwekezaji wa Pili: Achukue 15% – 20%.

Mwekezaji wa Tatu: Achukue salio la hisa zitakazobaki.

NOTE: Kama sehemu ya kuonyesha vitendo, Dr. Kigwangalla ametangaza kuwa kampuni yake ya HKGroup iko tayari kuingia mezani na kununua kati ya 9% hadi 15% ya hisa za Simba SC kwa fedha taslimu, endapo thamani ya hisa 49% za klabu hiyo ni TZS 20 Bilioni.

Mbali na kampuni yake, ameweka wazi kuwa ana uwezo wa kumleta mwekezaji mwingine mwenye uwezo wa kununua 15% hadi 20% kwa fedha taslimu mara moja.

Hili si suala la mtu mmoja. Ni suala la Simba ya kesho. Nguvu ya Simba isiwe kwa mtu mmoja; nguvu ya Simba iwe kwenye mfumo na iwe kwa Wanasimba," alihitimisha Kigwangalla.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI