Kassali kuivaa Coastal Union
Golikipa wa klabu ya Simba, Djibrilla Kassali ataukosa mchezo wa Ligi Kuu bara dhidi ya Pamba Jiji FC, baada ya golikipa huyo kuumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Taarifa ya Ahmed Ally, meneja habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba amesema baada ya kufanyiwa vipimo vya awali, imethibitika kassali ameumia goti (msuli wa pembeni ) na ripoti ya madaktari imeeleza jeraha lake sio kubwa na halihitaji upasuaji wa aina yoyote.
Kassali atarudi uwanjani kwenye mchezo unaofuata baada ya mchezo wa Pamba Jiji FC utakaochezwa jijini mwanza.
