Juma Mgunda amwadhibu Minziro
Wauaji wa Kusini, Namungo FC usiku huu imeibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Majaliwa Ruangwa mkoani Lindi mchezo wa Ligi Kuu bara dhidi ya Fountain Gate.
Bao pekee la Namungo limefungwa na Herbert Lukindo dakika ya 10, kwa matokeo hayo Namungo FC imefikisha alama 6 na ikiishusha Singida Black Stars inayokwenda nafasi ya saba.
Namungo inanolewa na Juma Mgunda wakati Fountain inanolewa na Fred Minziro.
