JKT Tanzania yafunga usajili na mchezaji wa Yanga

Klabu ya JKT Tanzania imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Offen Chikola kutoka Yanga SC, huku ikimtaja kama ‘X-Factor’ wa kikosi hicho kwa msimu wa NBC Premier League 2026/27.

JKT Tanzania imesema usajili huo umekamilika baada ya kukamilisha taratibu za kumpata Chikola, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya kikosi kwa msimu ujao.

“Kilio cha mashabiki wa JKT Tanzania kuwa wanataka X-Factor kimewafikia viongozi wetu wasikivu, nao wakasema mali hii itacheza JKT Tanzania FC msimu huu,” imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

Chikola amewahi kuzitumikia Singida Black Stars na Tabora United kabla ya kujiunga na Yanga SC.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI