Jayrutty atakiwa kuilipa Simba bilioni 5 za mkataba wake

Mzabuni CPA Joseph Rwegasira (@joerwegasira ) mkataba wake na Simba SC, Unamtaka kutoa kiasi cha Tsh. Shilingi Bilioni 5.7 (B.5.7) kwenye mwaka wake wa kwanza kiasi ambacho kitakuwa kinaongezeka kila mwaka kwa asilimia 10% ndani ya miaka mitano ambapo jumla itakuwa Bilioni 38.

JAYRUTTY mwaka wake ndani ya Simba SC hadaiwi kiasi chochote cha fedha ambacho kinamtaka kimkataba, JAYRUTTY mwaka wake wa kwanza amenunua Bus (Irizar) ambalo aliahidi kutokana na mkataba wake na Simba SC.

Lakini pia JAYRUTTY kwenye mwaka wake wa kwanza amesajili mchezaji (Inno Loemba) kitu ambacho hakipo Kimkataba ni Utashi wake tu mwenyewe.

Wachezaji kama Kassali, Anicet Oura, Libasse Gueye, Ismael Toure na Inno Loemba kila mmoja alinunuliwa gari na JAYRUTTY jambo ambalo halipo Kimkataba amefanya tu kwa mapenzi na utashi wake.

Sijajua wanaosema Mzabuni wa jezi JAYRUTTY hatoshi wanatumia nini kufikiri? Lakini pia sijui kwanini upande wa Tajiri MO DEWJI unamuona CPA Joseph Rwegasira kama tatizo wakati anaisaidia timu.? Sijui kabisa kwanini wanamuogopa JAYRUTTY.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI