Israel Mwenda hajatambulishwa Yanga!


Watu wanajiuliza Israel Patrick Mwenda yuwapi? Mbona hakutambulishwa miongoni mwa wachezaji takribani 35 sasa ambao Mabingwa wa nchi wamewatangaza?

Kwanza Israel Patrick Mwenda ni mchezaji wa Yanga mwenye mkataba wa miaka 2, yani mkataba wake utaisha msimu wa 2027-2028.

Pili, inadaiwa yapata miezi miwili sasa Israel alituhumiwa kupokea pesa na kutaka “Kuuza” mechi kutoka kwa timu moja ya Dar es Salaam.

Tatu, alipokea barua kutoka klabuni ikimuelekeza kusimama kazi ili kupisha tuhuma hizo nzito dhidi yake, kitu ambacho alikitii na ameendelea kutii.

Nne, tangu atuhumiwe hajaingiziwa mshahara wake kwa miezi hiyo 2.

Tano, klabu imemuandikia kumtaka arejee kambini na ikimuulizia kwanini haendi kambini.

Sita, mchezaji anasema kwakuwa alituhumiwa “Kuuza” ni vyema akaandikiwa barua inayomsafisha na tuhuma zile nzito manake jamii inazifahamu. Hajaandikiwa barua ambayo inasema nini matokeo ya uchunguzi na yeye amekutwa na hatia au hapana, kama hana hatia ni vyema klabu ikamuomba msamaha na kumtaka arejee kambini, sio kama ilivyo sasa ambapo ana andikiwa barua tu kumuulizia alipo na kwanini haingii kambini.

Saba, mchezaji anasema bila ya barua inayomuelezea hatima ya zile tuhuma hawezi kurudi, wenzie, wafanyakazi na mashabiki watamchukuliaje, atawaangaliaje?

Nane, msimamo wa klabu mpaka sasa unaonekana ni kutomlipa mshahara kwakuwa hayupo kazini.

Kwa mujibu wa mtoa habari jana Rais wa klabu ameongea na Baba wa mchezaji na amekiri tuhuma kwa mchezaji, uchunguzi haujamkuta na hatia, kweli hajalipwa mishahara miezi 2, hawawezi kumlipa mfanyakazi ambaye hayupo kazini, arudi kazini alipwe.

Kama alituhumiwa na kusimamishwa kazi alipaswa kulipwa mshahara wake wote kwa mujibu wa sheria za kazi, kutomlipa mshahara ni makosa, anaishije huyu ana familia na kazi yake soka?

Kama aliandikiwa barua ya tuhuma na kusimamishwa, kama hajakutwa na hatia, kwanini asiandikiwe barua ya kusema hatima ya uchunguzi na kumuomba msamaha ikimtaka arudi kundini ili kuweka rekodi zake sawasawa kama mfanyakazi. Picha ya mwanzo, huo ndiyo mtazamo wa wengi kwa Israel Patrick Mwenda kwa sasa


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI