Injinia Hersi awatoa wasiwasi Wanayanga
Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said, alitangaza rasmi uamuzi wa klabu hiyo kumuuza Allan Okello kuelekea msimu wa 2026/27.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa Stephane Aziz Ki, Hersi amesema mashabiki hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu kuondoka kwa Okello, akisisitiza kuwa milango ya Yanga itabaki wazi endapo mchezaji huyo atahitaji kurejea Jangwani.
Hersi Said: “Licha ya kwamba tumemuuza Okello, lakini hapa kwake ni nyumbani. Atarudi wakati wowote tukitaka kumrudisha au akitaka kurudi.”Okello alijiunga na Yanga Januari 2026 akitokea Vipers ya Uganda na ndani ya miezi saba aliweka alama kubwa, akimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa Yanga kwenye Ligi Kuu kwa mabao 14.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Okello ameuzwa kwenda ASFAR Rabat ya Morocco, klabu inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Pedro Gonçalves.
