Injinia Hersi amkabidhi jezi mbunge wa Bukombe
Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said, akimkabidhi jezi Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Doto Biteko zoezi lililofanyika katika Uwanja wa Bukombe kwenye uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi 2026.
Yanga SC ipo Ushirombo, Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita kwa ajili ya uzinduzi na maadhimisho ya Wiki ya Mwananchi ikiwa ni kwa mara ya kwanza kihistoria kwa tamasha hilo kufanyika nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
