Injinia Hersi amkabidhi gari mbunifu idara ya habari
Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, amemkabidhi zawadi ya gari Willy Shemoka @shemokawilly kama pongezi kwa kutokana na jitihada zake na ubunifu mkubwa alionesha kwenye idara ya habari.
Mafanikio haya yanaenda sambamba na ubunifu, bidii na maboresho makubwa katika uzalishaji wa maudhui ya Yanga.
Kama muandaa maudhui , Willy amekuwa sehemu muhimu ya safari hii, huku YouTube ya Yanga ikifikia hadhi ya kuwa namba moja Afrika kwa watazamaji. Hongera Willy Shemoka





