Ibrahim Jaabar avunja ukimya
Kiungo wa Simba SC, Ibrahim Jabaar, amevunja ukimya na kuonyesha ukomavu wa hali ya juu kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji FC jijini Mwanza.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Insta Story), nyota huyo ameonyesha uwajibikaji kwa kuandika ujumbe mfupi uliosomeka: "Hakuna visingizio, nawajibika kwa hili", akikubali kosa lililoiweka timu yake kwenye presha ya kucheza pungufu kipindi chote cha pili.
Kauli hiyo ya Jabaar inakuja muda mfupi baada ya Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally, kuweka wazi kuwa benchi la ufundi na uongozi utakaa na wachezaji kukemea rafu zisizo na ulazima zinazopelekea kadi nyekundu. Mwitikio huu wa Jabaar umepokelewa kwa hisia chanya na mashabiki wengi wa Msimbazi, wakimsifu kwa kuonyesha nidhamu, ukweli na ujasiri wa kukubali kosa badala ya kutafuta visingizio.
Unazungumziaje kitendo hiki cha Ibrahim Jabaar kukubali kosa na kuwajibika waziwazi kufuatia kadi hiyo nyekundu? Dondosha maoni yako!
