Hussein Abel kuwa kipa chaguo la kwanza Simba?

Golikipa namba mbili wa Simba, Hussein Abel ambaye leo katika uwanja wa Kaitaba Bukoba mkoani Kagera amechukua nafasi ya Mamadou Djibrila Kassali Tanja aliyeumia wakati timu yake ikiumana na Kagera Sugar.

Abel anaweza kuchukua nafasi na kuwa golikipa chaguo la kwanza endapo ataweza kuwajibika golini na kumshawishi kocha Steve Barker kusajili kipa mwingine endapo majibu ya daktari yatakuwa magumu kwa Kassali.

Kassali, amepata jeraha katika mchezo wa leo na hali yake imezua hofu baada ya kuonekana akilia uwanjani, jambo linaloashiria kuwa huenda majeraha hayo yakawa makubwa.

Kwa misimu kadhaa mfululizo, Simba imekuwa ikikumbwa na changamoto ya majeraha kwa makipa wake. Aishi Manula, Ayoub Lekred, Moussa Pinpin Camara na Yacoub Selemani ni miongoni mwa makipa waliowahi kukumbwa na majeraha yaliyowafanya kukaa nje kwa vipindi mbalimbali.

Hata hivyo, kuhusu hali ya Tanja Kassali, bado ni mapema kutoa hitimisho kuhusu ukubwa wa jeraha hilo.

Tunasubiri ripoti rasmi ya madaktari ili kufahamu hali yake na muda ambao anaweza kuwa nje ya uwanja.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI