Haruna Chanongo silaha ya Mashujaa FC
Mashujaa FC ya Kigoma Itanufaika sana kwa kuwa na huduma ya Kiungo Mshambuliaji, Haruna Chanongo mwenye umri wa miaka (32) kwa Mkataba wa mwaka mmoja akitokea Klabu ya Tanzania Prisons SC ya Jijini Mbeya.
Haruna Chanongo Amejiunga na Mashujaa FC akiwa Mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Tz Prisons SC, Nyota huyo Amewahi Kuzitumikia Klabu za Simba SC, Mtibwa Sugar, Pamba Jiji FC kabla ya Kujiunga na Tanzania Prisons SC ya Jijini Mbeya.
